LATEST NEWS

Friday, June 16, 2017

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KUWA MGENI RASMI MASHINDANO YA QU-RAN KIDUNIA YATAKAYOFANYIKA JUNI 18, MWAKA HUU JIJINI DAR

Jumla ya Washiriki 18 kutoka mataifa mbalimbali Duniani wanatarajia kushiriki fainali ya mashindano hayo yatakayo fanyika siku ya Ijumapili Juni 18, 2017 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es salaam.

Kwamujibu wa Mjumbe wa kamati inayo Ratibu Mashindano hayo Thabit Badi amesema mpaka sasa wameshawasili washiriki 15 na mpaka kufikia saa nane usiku kuamkia kesho watakuwa wamewasili wote.

Katika Fainali hiyo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasim Majaliwa anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi.Washiriki wa mashindano hayo wakiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
Mjumbe wa kamati inayo ratibu Mashindano ya Qu-ran, Thabit Badi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya Mashindano ya Qu-ran yatakayofanyika siku ya Ijumapili Juni 18, mwaka huu katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment

Adbox