Mabingwa wa ligi kuu ya Kenya Gor Mahia jana usiku
walilambishwa sakafu na timu ya Everton kutoka Uingereza katika mechi ya
kirafiki iliyochezwa uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United Wayne Rooney na
kiungo Kieran Dowell walipachika bao moja kila moja na kusaidia Everton
kuzima Gor Mahia 2-1.
Timu zote zilianza vizuri kabla ya Gor kuimarika. Hata hivyo, Everton
ilizidi nguvu Gor, ambayo ilijikatia tiketi ya kumenyana na klabu hiyo
ya Uingereza baada ya kuaibisha mahasimu wa jadi AFC Leopards 3-0 katika
fainali ya shindano la SportPesa Super Cup nchini Tanzania hapo Juni
11.
No comments:
Post a Comment