LATEST NEWS

Friday, July 14, 2017

Askari wa Kenya wawaokoa watu waliotekwa nyara na wapiganaji wa Al-Shabaab

Askari wa Kenya jana wamewaokoa watu sita waliotekwa nyara na kundi la Al Shabaab mjini Lamu, akiwemo ofisa mmoja wa serikali.
Msemaji wa jeshi la ulinzi la Kenya Kanali Joseph Owuoth amesema, katibu wa kudumu wa wizara ya ujenzi Bi. Maryam El Maawy ameokolewa kwenye operesheni hiyo ambapo gari lake lilipinduka mara kadhaa na kulipuka. Polisi wa eneo hilo wamesema, watu wasiopungua watatu wameuawa akiwemo dereva, na katibu huyo alipigwa risasi kwenye bega na mguu wakati wa operesheni ya uokoaji.
Awali, Kamanda wa polisi wa mkoa wa Pwani James Akoru amesema, watu sita walitekwa nyara na wapiganaji 30 wenye silaha nzito katika eneo la Milihoi, barabara kuu ya Lamu-Mpeketoni.

No comments:

Post a Comment

Adbox