LATEST NEWS

Monday, July 3, 2017

MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA MKUTANO WA 29 wa UMOJA WA FRIKA MJINI ADDIS ABABA

Mkutano
wa 29 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU)
amefunguliwa rasmi Jijini Addis Ababa- Ethiopia ambapo Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli anawakilishwa na Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan
katika mkutano huo

Mkutano huo wa Wakuu wa Nchi na Serikali
unaofanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika Jijini Addis Ababa-
Ethiopia na utajikita katika kujadili masuala mbalimbali yanayohusu
umoja huo ikiwemo hali ya ulinzi na usalama katika Bara la Afrika hasa
kwenye nchi za Sudan Kusini, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo-
DRC na Libya.

Aidha, Viongozi hao watajadili hali ya usalama
kwenye baadhi ya nchi ambazo ziliathiriwa na kundi la Boko Haram za
Nigeria, Niger, Chad na Cameroon.

Wakuu hao wa Nchi na Serikali
wa AU pia watajadili kwa kina kuhusu uanzishwaji wa eneo huru la
kibiashara katika bara la Afrika kwa ajili ya kuliendeleza Bara hilo kwa
ajili ya kukuza biashara baina ya nchi wanachama, uwekezaji, kuondoa
vikwazo vya kibiashara pamoja na kupunguza utegemezi kwa masoko ya nje.

Mambo
mengine yatakayojadiliwa na Viongozi hao ni bajeti ya Umoja huo, mpango
mkuu kuhusu hatua za kivitendo za kuzuia mapigano katika Afrika
kufikia mwaka 2020, maboresho katika Baraza la Usalama la Umoja wa
Mataifa na maboresho ya kitaasisi katika AU.

Kwa upande wa
Tanzania, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan anaongoza ujumbe wa
Tanzania katika mkutano huo ambao unahudhuriwa pia na Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Augustine Mahiga na Waziri
wa Kazi,Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar Maudline Cyrus Castico pamoja na Watendaji wengine
wa Serikali. Kauli Mbiu ya Mkutano wa mwaka huu ni Kuimarisha
Mgawanyiko wa Idadi ya Watu Kupitia Uwekezaji katika Vijana. (Harnessing
Demographic Divident Through Investments in the Youth)

Picha ya pamoja

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amemwakilisha Rais wa John Pombe Magufuli katika mkutano wa AU katika Makao makuu ya Umoja huo Addis Ababa- Ethiopia.Mkutano umefunguliwa hii Leo Jijini Addis Ababa- Ethiopia.

Mkutano wa AU katika Makao makuu ya Umoja huo Addis Ababa- Ethiopia uliofunguliwa leo hii eo Jijini Addis Ababa- Ethiopia ukiendelea

No comments:

Post a Comment

Adbox