Barcelona wamekamilisha usajili wa mshambualiji wa Borrusia Dortmund Ousmane Dembele kwa uhamisho wa kitita cha pauni 135.5milioni.
Mchezaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 20 ametia saini kandarasi ya miaka mitano katika uwanja wa Nou Camp akiwa na rais wa klabu hiyo Josep Maria Bartomeu.
Kandarasi hiyo ni ya pili kwa thamani baada ya ile ya hivi karibuni ya Neymar kuelekea PSG iliogharimu pauni milioni 200. Mara ya mwisho kwa Dembele kuichezea Dortmund ni wakati wa kombe la Supercup mnamo tarehe 5 mwezi Agosti.
No comments:
Post a Comment