LATEST NEWS

Wednesday, August 30, 2017

Mwanariadha wa Marekani afariki dunia

Mwanariadha wa mbio za masafa ya wastani kutoka Marekani David Torrence mwenye umri wa miaka 31 amepatikana amefariki katika bwawa la kuogelea katika jimbo la Arizona

Torrence alishinda fedha katika mbio za ubingwa wa dunia za kupokezana vijiti mwaka 2014 na alimaliza wa pili pia katika mbio za bara la Amerika mwaka 2015.

Alibadilisha uraia kutoka Marekani hadi Peru na akawakilisha taifa hilo lake jipya katika michezo ya Olimpiki ya Rio mwaka 2016.

Taarifa ya polisi imesema kwamba hakuna dalili zozote dhahiri kwamba huenda aliuawa.

No comments:

Post a Comment

Adbox