Klabu ya Arsenal inasemekana tayari wamekubali ofa kutoka Manchester City kwa ajili ya kumnunua mshambuliaji Alexis Sanchez kutoka Arsenal, City walituma kiasi cha £60m na inaonekana Gunners wamekubali.
Divock Origi amejiunga na klabu ya soka ya Wolfburg inayoshiriki ligi kuu soka ya Bundesliga, Origi amesaini mkataba wa kuichezea klabu hiyo kwa mkopo akitokea Liverpool.
Klabu ya Chelsea baada ya kutoswa na Oxlade Chamberlain aliyesaini Arsenal sasa wamekubali kutoa pesa kwa Lazio kumnunua mlinzi Davide Zappacosta na dili hilo linaonekana tayari limeshakamilika.
Hadi sasa haijaeleweka ni wapi winga Ryad Mahrez anaelekea, kwani ilisemekana yuko Hispania kukamilisha uhamisho wa kujiunga na Barcelona lakini klabu hiyo imesema haina mpango wa kumnunua, sasa Arsenal na Chelsea wanapewa nafasi kubwa kumnunua.
Klabu za Paris Saint German na Monaco zimebadili makubaliano kuhusu usajili wa Mbappe, hapo mwanzo ilitakiwa Mbappe aende PSG kwa mkopo lakini sasa anauzwa kabisa kwa dili litakaloigharimu PSG kiasi cha £140m.
Klabu ya Liverpool imekanusha taarifa zilizozagaa kwamba kiungo wao Phellipe Coutinho atasaini Barcelona usiku wa leo, Liverpool wamesema huo ni uzushi na Coutinho atabaki kuwa mchezaji wao.
Thursday, August 31, 2017
Kinachoendelea hivi sasa katika siku ya mwisho ya usajili barani Ulaya
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment