LATEST NEWS

Thursday, August 31, 2017

Askofu wa kanisa Katoliki awapa hifadhi wakimbizi 2,000 Wiislamu nchini CAR

Walinda amani wa Umoja wa mataifa, wamekuwepo nchini humo tangu mwezi Aprili mwaka 2014

Askofu mmoja wa kanisa Katoliki katika Jamhuri ya Afrika ya Kati-CAR, amewapa hifadhi zaidi ya waislamu 2,000, ambao wanaishi kwa hofu ya kushambuliwa na kundi moja kuu la wanamgambo wakristo, nchini humo.

Juan José Aguirre Munoz, anasema wakimbizi hawawezi kutoka katika uwanja wa kanisa hilo lililoko Kusini Mashariki mwa mji wa Bandassou.
 
Wiki iliyopita, afisa mkuu wa umoja wa mataifa wa kitengo cha utoaji msaada wa kibinadamu, alitoa tahadhari ya uwezekano wa kutokea mauwaji ya kimbari. Stephen O'Brien, amesema kuwa vurugu inazidi kuongezeka huku hali ikiwa mbaya zaidi nchini humo.

Jamhuri ya Afrika ya Kati, imeshuhudia ghasia mapigano mabaya zaidi tangu mwaka 2013, wakati kundi kubwa la waasi wa kiislamu- Seleka lilipochukua utawala wa nchi hiyo, na kulaumiwa kuwa limekuwa likiauwa watu wasio waislamu.

No comments:

Post a Comment

Adbox