Mbwembwe za bondia Floyd Mayweather sasa zimevuka mipaka baada ya jana kuiomba Kamati ya Mashindano ya Ngumi Nevada (NAC) kutumia glovu nyepesi kwenye pambano dhidi ya mpinzani wake, Conor McGregor litakalofanyika Agosti 26.
Mabondia hao walitakiwa kuwasilisha vifaa watakavyotumia siku ya pambano juzi ili kuhakikiwa na kamati hiyo, badala yake akaomba kutumia glovu zenye uzito mdogo ili kumsulubu mpinzani wake.
Kamati hiyo ilisema kwa mujibu wa NAC kila pambano lina glovu za uzito wake, hivyo suala la kupunguza ukubwa wa glovu hizo linahitaji mjadala ambao utapatiwa ufumbuzi Agosti 16.
Glovu nyepesi humfanya mpiganaji kuwa mwepesi kurusha ngumi jambo ambalo linaweza kumpa bondia kuwa mwepesi kupangua makombora au kumshinda mwenzake kirahisi.
No comments:
Post a Comment