Ikiwa dirisha la usajili Ulaya linaelekea kufungwa, nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta amezungumzia kuhusu tetesi zilizo mhusisha kujiunga na klabu ya Fenerbahçe inayoshiriki ligi kuu ya Uturuki.
Fenerbahçe walitajwa kutaka kumsaini Samatta kutokea KRC Genk anayoichezea kwa sasa nchini Ubelgiji ili kuziba nafasi ya mshambuliaji wao Robin van Persie ambaye umri wake umekimbia kwa sasa.
Baada ya mazoezi yake ya pamoja na kikosi cha timu ya taifa kinachojiandaa na mchezo dhidi ya Botswana uliyopo katika kalenda ya FIFA yaliyofanyika jana Mbwana Samatta alikataa katakata kuongelea suala hilo akisema liko nje ya uwezo wake na hawezi kulizungumzia.
No comments:
Post a Comment