Teknolojia imekuwa kubwa siku za usoni na watu wanatumia
mitandao ya kijamii kurahisisha mawasiliano yao, lakini mitandao hiyo
hiyo wapo wanaoitumia vibaya na kuleta machafuko.
Wahalifu wa mitandao walifanikiwa kuiba account ya mshambuliaji wa
Manchester United Romelu Lukaku, hawakuishia hapo tu bali walienda mbali
zaidi na kufanya jambo linaloweza kuleta ugomvi kati ya Lukaku na
Cristiano Ronaldo.
Baada ya tukio la Ronaldo kumsukuma muamuzi katika mchezo wa El
Classico na kupewa adhabu ya kukaa nje michezo mitano, Ronaldo aliandika
mtandaoni kutovutiwa kwakwe na maamuzi ya tukio hilo.
Sasa wakati Cristiano akijitetea kupitia Instagram account yake kati
ya watoa maoni wa tukio hilo mmoja wapo alikuwa ni Lukaku ambaye
aliandika Lioneil Messi ni bora kuliko Cristiano Ronaldo.
Baada
ya muda comment hiyo ilifutwa lakini watu walishaiona, ilibainika
kwamba hakuwa Lukaku aliyeandika hivyo bali account yake iliibiwa
japokuwa hadi sasa Lukaku mwenyewe hajaongea lolote kuhusiana na tukio
hilo.
Thursday, August 31, 2017
Vibaka wa mitandaoni almanusra wawaingize Cr7 na Romelu Lukaku katika mzozo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment