LATEST NEWS

Wednesday, August 30, 2017

Mark Zuckerberg amtaka bintiye awe akitoka nje kucheza

                     Picha ya familia ya Bwana na Bi Zuckerberg na watoto wao wawili 

Mwanzilishi wa mtandao wa kijamii wa Facebook, tajiri Mark Zuckerberg, amemsihi bintiye mdogo kuwa akitoka nje kucheza nje na kufurahia maajabu ya kuwa mtoto, katika barua yenye hisia iliyochapishwa katika ukurasa wake katika mtandao wake wa Facebook.

Barua hiyo ilichapishwa siku ya Jumatatu alipotangaza kuzaliwa kwa mwanawe wa pili aitwaye August, na mkewe Priscilla Chan.

Katika barua ya kina waliyoiandika, wazazi hao wawili walizungumzia kuhusu maajabu ya kuwa mtoto na umuhimu wa kucheza.

Wawili hao waliweka mtandaoni barua kama hiyo kwa binti yao Max mnamo mwaka 2015.

Katika ujumbe hao ambao ameuambatanisha na picha ya familia, Bw Zuckerberg, pia amemhimiza mgeni huyo mchanga "asiwe mkubwa kwa haraka".

"Dunia inaweza kuwa eneo la ushindani mkali. Hiyo ndiyo maana ni muhimu kutafuta nafasi na kwenda nje ili kucheza," ilisema barua hiyo, iliyotiwa saini "Mom and Dad", yaani ''Baba na Mama ''

Wito wa mtoto kwenda kujitambua nje ya nyumba unaonekana kwenda kinyume na lengo kuu la mtandao wa bilionea huyo anayemiliki kampuni kubwa ya mtandao wa kijamii duniani ambaye mara kwa mara hutoa wito wa watu kutumia zaidi mitandao ya kijamii kufahamiana na kujumuika pamoja.

"Matumaini yangu ni kwamba ukimbie mara nyingi sana na kuzunguka sebuleni na pia huko nje kadiri utakavyotaka. Na kisha, natumai kwamba utalala sana," wazazi hao wawili waliandika.

"Utotoni ni hatua nzuri sana. Huwa wawa mtoto mara moja tu, kwa hivyo usitumie muda mwingi sana kufikiria sana kuhusu mustakabali wako."

No comments:

Post a Comment

Adbox