Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, TAKUKURU imewafikisha katika Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu vigogo watano wa zamani wa Shirika la Umeme
Tanzania, Tanesco wakidaiwa kuhujumu uchumi kwa kuisabishia Serikali
hasara ya Tsh. Milioni 275.
Waliofikishwa
Mahakamani ni pamoja na aliyekuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco,
Robert Shemhilu, Ofisa Ugavi, Harun Mattambo, Mkurugenzi wa Fedha,
Lusekelo Kasanga, Mwanasheria wao, Godson Makia pamoja na msambazaji
kutoka kampuni ya M/S Young Dong Electronic Co. Ltd Martin Simba.
Wakili
wa Serikali, Vitalis Peter aliwasomea washtakiwa hao mashtaka mawili ya
uhujumu uchumi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba ambapo alidai
kuwa kati ya January na December 2011 katika Ofisi za Tanesco Ubungo,
washtakiwa wakiwa waajiriwa wa Shirika hilo, walitumia madaraka yao
vibaya kwa kufanikisha malipo kwa msambazaji Martin Simba bila ya
kufanya uhakiki.
Aidha,
Wakili Vitalis amedai kati ya January na December 2011 katika Ofisi za
Tanesco Ubungo, washtakiwa hao wakiwa waajiriwa wa shirika hilo pamoja
na msambazaji huyo waliisababishia Serikali hasara ya Tsh. Milioni 275.
Baada
ya kusomewa mashtaka hayo washtakiwa waliruhusiwa kuongea kwa sababu
Mkurugenzi wa Mashtaka DPP amewasilisha Cheti maalum kinachoiruhusu
Mahakama kuisikiliza kesi hiyo ambapo walikana na upande wa mashtaka
ulidai kuwa upelelezi umekamilika.
Hakimu
Simba aliwataka washtakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika ambao
kila mmoja alisaini bondi ya Tsh. Milioni 40 huku mmoja kati ya
wadhamini hao akitakiwa kuwasilisha hati ya Mali isiyohamishika ambapo
walitimiza masharti hayo.
Washtakiwa hao watasomewa maelezo ya awali (PH) August 24, 2017.
No comments:
Post a Comment