Jeshi la Polisi Dodoma linawashikilia watu 11 kwa uchunguzi
kutokana na mauji ambapo August 8, 2017 majira ya saa 4:00 usiku katika
kitongoji cha Chang’ombe Wilaya ya Chamwino mtu mmoja mwanamke
aliyefahamika kwa jina la Mariam Saidi miaka 17 mkazi wa Kigoma aliuawa
kwa kukatwa shingo na kutenganishwa na kiwiliwili na kuchomwa moto.Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Dodoma Lazaro Mambosasa wakati akiongea na waandishi
wa habariMwili wa marehemu ulikutwa nyumbani kwa mganga wa jadi aitwaye
Ashura Mkanga mwenye miaka 33 na mkazi wa kitongoji cha Chang’ombe
ambapo mazingira ya tukio yanaonesha kuwa mganga huyo wa jadi asiye na
kibali kuendesha shughuli za tiba asili analaza wagonjwa nyumbani kwake,
anafanya matambiko, anapiga ramli chonganishi, anafanya tohara za
watoto katika nyumba yake pamoja na matambiko.
“Tukio hili ni baya na halikubaliki hapa Dodoma na
mahala popote, ni fedheha kubwa sana kwa wananchi kuendelea kukumbatia
imani za kishirikina katika karne hii na Serikali imesogeza huduma za
afya karibu na jamii lakini bado wapo watu hawataki kwenda hospitali na
kukubali kuuawa kwa fedheha na waganga wachonganishi.” Alisema Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Lazaro Mambosasa wakati akiongea na waandishi wa habari
No comments:
Post a Comment