LATEST NEWS

Friday, September 8, 2017

Madaktari watoa meno 7 kutoka kwa mtoto wa mwezi mmoja India

 
Madaktari kwenye hospitali moja iliyo jimbo la magharibi mwa Inida ya Gujarat wamefanikiwa kutoa meno saba kutoka kwa mtoto wa mwezi mmoja.

"Kwa sasa mtoto yuko sawa," daktari ambaye alifanya upasuaji huo Meet Ramatri alisema.

Alisema kuwa upasuiji huo ulifanya kwa njia mbili. Kwanza walitoa meno manne, na baadaye matatu.

Meno ya mtoto huyo yaligundulwia siku chache baada ya kuzaliwa.

Wazazi wake walimpeleka kwa daktari wakati alipata matatizo ya kunyonya,

 

 Baada ya kumfanyia uchunguzi dakari aligundua nyama nyeupe na kumtuma kwa daktari Ramatri.

"Wakati nilimfanyia uchunguzi aligundua meno saba,"


Kisha alilazimika kutoa meno hayo kwa njia ya upasuajia.

"Sasa mtoto huyo anaweza kunyonya," dakatari alisema, lakini aliongeza kuwa ni vigumu kujua ikiwa upasuaji huo utatatiza ukuaji wa meno ya mtoto huyo siku za usoni


#BBC SWAHILI

No comments:

Post a Comment

Adbox