LATEST NEWS

Tuesday, September 5, 2017

Polisi yamkabidhi Manji kwa Mahakama


   

Polisi imemkabidhi mfanyabiashara Yusuf Manji (41) na wenzake watatu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kumaliza kuwahoji kuhusu kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili. Jana, Septemba 4 Mahakama iliruhusu washtakiwa kwenda kuhojiwa polisi kwa ajili ya kukamilisha upelelezi.

Hata hivyo, tofauti na jana alipovaa suti, leo Septemba 5 Manji amefika mahakamani na vazi lake la zamani la fulana nyeusi na suruali nyeusi. Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi amedai wamewarudisha washtakiwa kama walivyoamriwa na Mahakama.

Upande wa mashtaka ulitakiwa kuwarudisha muda wa kazi baada ya kuhojiwa polisi. Mbali na Manji, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Meneja Rasilimali watu wa Kampuni ya Quality Group Ltd, Deogratius Kisinda (28), mtunza stoo, Abdallah Sangey (46) na Thobias Fwere (43), mkazi wa Chanika wanakabiliwa na mashitaka ya uhujumu uchumi.

Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi ameahirisha kesi hadi Septemba 8

No comments:

Post a Comment

Adbox