Watuhumiwa hao wakiwa katika viunga vya Mahakama ya Kisutu,mapema leo kwenye kesi yao ya kudaiwa kujihusisha na biashara ya meno ya tembo,ambayo kwa sasa inatarajiwa kupelekwa Mahakama ya mafisadi. |
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa, hati ya mashtaka ya kesi ya
kujihusisha na biashara ya meno ya tembo dhidi ya mfanyabiashara Yusuf
Alli maarufu kama mpemba wa Magufuli’ inatarajiwa kupelekwa Mahakama ya
mafisadi.
Hayo yameelezwa na wakili wa serikali, Elia Athanas
mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba kesi hiyo ilipokuja kwa
kutajwa. "Mheshimwa, jalada la kesi hii limekamilika, hivyo naomba muda
ili wapeleke hati ya mashtaka Mahaka Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu
Uchumi 'Mahakama ya Mafisadi'.
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi September 19/2017.
Yusuf anashtakiwa pamoja na Charles Mrutu, mkazi wa Mlimba, Morogoro,
Benedict Kungwa, mkazi wa Mbagala Chamazi, Jumanne Chima, mkazi wa
Mbezi, Ahmed Nyagongo, dereva na Pius Kulagwa, wanakabiliwa na mashitaka
manne ya kujihusisha na biashara ya meno ya tembo yenye thamani ya
Sh.milioni 785.6.
Inadaiwa katika tarehe tofauti kati ya Januari,
2014 na Oktoba, mwaka huu wakiwa Dar es Salaam, Tanga, Iringa na
Mtwara, walijihusisha na mtandao wa ujangili kwa kukusanya na kuuza
nyara za serikali ambazo ni
vipande 50 vya meno ya tembo vyenye
thamani ya Dola za Marekani 180,000 sawa na Sh milioni 392.8 bila kuwa
na kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori.
Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.
No comments:
Post a Comment