LATEST NEWS

Wednesday, September 6, 2017

SAFARI YA MWISHO YA MWANAHABARI MKONGWE NA ALIYEWAHI KUWA DC, MAREHEMU MUHINGO RWEYEMAMU

Jeneza lenye Mwili wa marehemu, Muhingo Rweyemamu aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilayaka katika Serikali ya awamu ya nne na Mwandishi wa habari mkongwe nchini, ukiwa kwenye viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuagwa, mchana wa leo kabda ya mazishi yake yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kinondoni.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza kabla ya kuongoza waombolezaji katika kuaga mwili wa marehemu, Muhingo Rweyemamu mcahan wa leo kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Marehemu Muhingo Rweyemamu amezikwa leo kwenye makaburi ya Kinondoni.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akitoa neno wakati wa kumuaga Mwandishi wa habari mkongwe nchini, Muhingo Rweyemamu yaliyofanyika leo Uwanja wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Mtoto wa marehemu akisoma risala.


Mwili wa marehemu mwandishi wa habari mkongwe nchini, Muhingo Rweyemamu ukiingizwa uwanja wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.





Waombolezaji wakiwa katika uwanja wa mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Tanga Godwin Gondwe akitoa machache.




Familia na viongozi waliowahi kufanyakazi na marehemu mwandishi wa habari mkongwe nchini, Muhingo Rweyemamu.

Mhariri Mtendaji wa kampuni ya New Habari, Absalom Kibanda akitoa neno la shukrani kwa wanaombolezaji.






Viongozi na waombezaji wakioaga mwili wa marehemu.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akiongea na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda mara baada ya kuaga mwili wa marehemu.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akisalimiana na mwandishi mkongwe Hamis. 
MICHUZI

No comments:

Post a Comment

Adbox