Maafisa katika jimbo la Texas nchini Marekani wameripoti kuwa watu 60 wameaga dunia katika kimbunga cha Harvey kilicholiathiri pakubwa jimbo hilo.
Maafisa hao wamebainisha kuwa wahanga wengi wa kimbunga cha Harvey wameghiriki katika maji mengi ya mafuriko yaliyojaa katika mitaa ya jimbo la Texas.
Kimbunga cha Harvey pia kimesababisha kaya laki tano kusini mashariki mwa Texas kukosa makazi huku taasisi za kushughulikia maafa za Marekani zikitangaza kusajili karibu kaya 560,000 kwa ajili ya kuwapatia makazi. Ripoti mbalimbali zinaeleza kuwa kimbunga cha Harvey kimebomoa pia nyumba elfu 40 na kuharibu magari milioni moja. Hasara ya kimbunga cha Harvey jimboni Texas
Wabunge wa Baraza la Wawakilishi la Marekani na Seneti ya nchi hiyo pia wanatazamiwa kupiga kura kwa ajili ya kuyasaidia maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga hicho huko Texas. Si huko Texas pekee, bali kimbunga cha Harvey kimesababisha maafa na hasara kubwa kwa miundombinu ya sekta ya mafuta na gesi asilia katika jimbo la Lousiana pia.
No comments:
Post a Comment