LATEST NEWS

Thursday, September 7, 2017

TANESCO Mkoani Singida kuwasaka wanaoiba umeme mkoani humo



SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Singida limeanza zoezi la kuwasaka na kuwakamata wateja wanaojiunganishia nishati ya umeme bila kufuata utaratibu uliowekwa na shirika hilo na hivyo kuchangia kutumia huduma hiyo bila kulipia na hivyo kulikosesha shirika mapato.

Aidha katika kipindi cha kuanzia julai hadi Sept,03, mwaka huu shirika hilo limeshafanya ukaguzi kwa wateja 646 wa Kata ya Itigi na Mwamagembe,wilayani Manyoni.

Akitoa taarifa ya zoezi hilo Meneja wa TANESCO Wilaya ya Manyoni, Patrick Mtukananje amesema kati ya wateja hao 646, wateja 312 walibainika kuwa na matatizo na wateja 334 wamegundulika kuwa hawana matatizo yeyote dhidi ya tuhuma walizokuwa wakikabiliwanazo.

Aidha Meneja huyo amemtaja mtumishi wa shirika hilo anayetumiwa kuhusika na ukiukwaji wa taratibu hizo za shirika kuwa ni aliyekuwa msimamizi wa Kituo cha Itigi,Rajabu Ramadhani na kwamba mpaka sasa ameshasimamishwa kazi na anatarajiwa kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

No comments:

Post a Comment

Adbox