LATEST NEWS

Thursday, September 7, 2017

Wananchi wa mji wa Kahama wameomba kufungwa kwa ofisi ya mtendaji wa kata ya Mhongolo kwa ubadhilifu wa mali za umma unaofanywa na viongozi wa ofisi hiyo.



Na Alfred Bulahya KAHAMA

Wananchi wa mtaa wa mbulu kata ya mhongolo halmashauri ya mji wa Kahama wamemuomba diwani wa kata hiyo Maiko Mizubo kufunga ofisi ya mtendaji wa mtaa huo kwa kile kinachodaiwa kuwepo ubadhilifu wa mali za umma unaofanywa na viongozi wa ofisi hiyo.

hatua hiyo imefikiwa na wananchi hao katika mkutano wa hadhara baina yao na viongozi mbalimbali akiwemo diwani wa kata hiyo uliokuwa umelenga kusoma taarifa ya mapato na matumizi ya mtaa huo.

Wamesema kuwa wanamuomba diwani huyo kufunga ili kusitisha huduma katika ofisi hiyo ili kupisha uchunguzi, jambo ambalo litasaidia kuepusha kubadilishwa kwa mihutasari mbalimbali iliyopo ofisini hapo.

hata hivyo diwani wa kata hiyo Maiko Mizubo amesema kuwa hawezi kufunga ofisi hiyo kwani hana mamlaka ya kufanya hivyo huku akiwaomba wananchi kusubiri viongozi kutoka katika ngazi za juu watakaoweza kumaliza tatizo hilo.

Naye afisa mtendaji wa kata hiyo amesema kuwa mnamo august 25 mwaka huu walifanya kikao cha wdc ili kujadili changamoto hizo kisha kuleta changamoto hizo katika mkutano huo na kwamba amewaomba wananchi kuwa wavumilivu kwani jambo hilo linashughulikiwa.

Aidha mkutano huo umeshindwa kutatua changamoto hizo kutokana na hali ya mzozo huo kujitokeza ndipo mwenyekiti wa mtaa huo akaamua kufunga mkutano huo huku akiahidi kuitisha mkutano wa hadhara siku nyingine.

No comments:

Post a Comment

Adbox