Wednesday, October 18, 2017

Mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China wafunguliwa


Mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China umefunguliwa leo Beijing nchini China. Katibu mkuu wa Kamati kuu ya chama Bw. Xi Jinping kwa niaba ya Kamati kuu ya 18 ya chama ametoa ripoti kuhusu mpango wa jumla wa maendeleo ya China katika siku za baadaye kwenye mkutano huo.

Zaidi ya wajumbe 2000 waliochaguliwa kutoka wanachama milioni 89 wa Chama cha Kikomunisti cha China, wamethibitisha ripoti ya Bw. Xi Jinping, na ripoti ya kazi ya kamati kuu ya ukaguzi wa nidhamu ya awamu iliyopita, kujadili mswada wa marekebisho ya katiba ya chama, na kuchagua kamati kuu ya awamu mpya ya chama na kamati kuu ya ukaguzi wa nidhamu ya awamu mpya.

#CRI

No comments:

Post a Comment

Adbox