Baadhi ya wanawake wa halmashauri ya mji wa Babati Mkoani Manyara wameeleza umuhimu wa taasisi zinazoendesha zoezi la uchunguzi wa magonjwa yasiyoambukiza kama vile saratani ya mlango wa kizazi kupanua huduma hadi vijijini.
Magreth Kimei ametoa ushauri huo wa kufanyiwa uchunguzi ili wale watakaogundulika kuanza kuchukua hatua za kuokoa maisha yao hususani wasiofahamu dalili za ugonjwa huo yakiwemo makundi ya wanawake wanauza miili yao,wanaume wenye wanawake wengi na ndoa za mitaala.
Akizungumzia katika zoezi la kujitolea lililoloendeshwa na Chama Cha kupambana na magonjwa yasiyoambukiza Mkoa wa Manyara Dk Nicodemus Kaje alieleza kuwa magonjwa wanayoyaangalia zaidi ni kisukari,shinikizo la damu na saratani ya mlango wa kizazi ambapo asilimia 3 ya wanawake Tanzania hukumbwa na tatizo hilo.
No comments:
Post a Comment