LATEST NEWS

Friday, March 31, 2017

Serengeti Boys yatakata yaitandika Burundi magoli matatu

 
Timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 Serengeti Boys imeibuka na ushindi wa mabao Matatu kwa bila dhidi ya Burundi katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliochezwa kwenye uwanja wa Kaitaba mkoni Kagera.

Serengeti Boys inayojiandaa na fainali za kombe la Afrika kwa vijana mchezo utakaofanyika nchini Gabon mwezi Mei na itacheza mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya Ghana siku ya jumatatu kwenye uwanja wa taifa jijini DSM.

Mchezo huo utatumika kuiaga  timu hiyo kabla ya  kwenda Morocco kuweka kambi ya mwezi mmoja kujiandaa na fainali nchini  Gabon.

No comments:

Post a Comment

Adbox