Serikali ya Tanzania imekanusha
taarifa ambazo zimekuwa zikienea katika mitandao ya kijamii na baadhi ya
vyombo vya habari kwamba Rais Magufuli aliamuru Wakenya wanaoishi
upande wa Tanzania katika mji wa mpakani wa Namanga watimuliwe.
Tanzania imeiomba serikali ya Kenya kupuuzilia mbali taarifa hizo na badala yake, nchi hizo mbili "ziangazie kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na kibiashara ambao umekuwepo."
Taarifa hizo zilisababisha maandamano na vurugu katika mji huo mapema wiki hii, Wakenya wakilalamika.
Shughuli za kiserikali na za kibiashara katika mji huo zilitatizwa na vurugu hizo, sana Jumatatu.
Katibu katika wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt Aziz Mlima amesema taarifa hizo ni za uongo.Amesema lengo la taarifa hizo ni "kumharibia Rais Magufuli sifa zake nzuri ambazo amejizolea kufikia sasa pamoja na picha nzuri ya Tanzania kwa jumla."
Dkt Aziz hata hivyoa amesema sheria za uhamiaji ni sharti zifuatwe.
Amesema wizara ya mambo ya nje ya Tanzania ilifanya operesheni ya kuwatimua wageni, wakiwemo Wakenya, wanaoishi Tanzania bila vibali vya kuishi au kufanyia kazi nchini humo.
SourceBBC News
No comments:
Post a Comment