LATEST NEWS

Sunday, April 23, 2017

Sare za polisi, askari wa jiji Arusha mkanganyiko tupu

Image result for sare za askari jiji la arushaHalmashauri ya Jiji la Arusha imetoa ufafanuzi wa sare zinazotumiwa na askari wake zinazofanana za Idara ya Uhamiaji ikisema zimepitishwa kwa kuzingatia utaratibu wa ulinzi.

Imeelezwa sare hizo zimepata kibali cha Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Ernest Mangu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Athumani Kihamia akizungumza na gazeti hili juzi alisema kwa mujibu wa sheria, jiji linapaswa kuwa na Askari Wasaidizi (Auxiliary Police) badala ya mgambo na wamefuata utaratibu kufikia hatua hiyo ambayo inaonekana ni jambo geni kwa wananchi wengi.


Alisema halmashauri imetumia Sh72 milioni kuwapa mafunzo ya kijeshi askari 28 kwa kipindi cha miezi sita yaliyotolewa Mikumi mkoani Morogoro na baada ya kuhitimu walipeleka aina ya sare watakayoitumia ofisi ya IGP na kukubaliwa.
“Baada ya kupata kibali kutoka kwa IGP tuliipeleka pia kwenye kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ambayo nayo iliafiki kuwa sare rasmi ya askari wa jiji.


“Jambo linalosumbua kwa sasa ni kwamba, baada ya kuanza kazi majukumu yao yamepungua na hasa katikati ya mji ambako wananchi wangekuwa wamewazoea lakini kwa sasa tumewagawa kwenye kata ili kuimarisha ulinzi huko,” alisema Kihamia

Ufafanuzi huo umetolewa baada ya baadhi ya wananchi kuona kuna mlingano wa sare za Idara ya Uhamiaji na Askari wa Jiji la Arusha jambo lililojadiliwa kwenye mitandao ya kijamii siku tatu zilizopita baada ya picha ya askari kuwekwa kwenye moja ya mitandao ya kijamii ya gazeti hili.

Mkazi wa Kwamrombo jijini hapa, Dorcas Jonathan alisema kumekuwa na mkanganyiko kutokana na wananchi kuzoea sare za mgambo.
source: Mwananchi

No comments:

Post a Comment

Adbox