Friday, March 31, 2017

Wachina 28 washikiliwa Uganda kwa kuishi na kufanyakazi nchini humo bila vibali

Raia wa China wamekamatwa nchini Uganda wakiwa hawana vibali vya kufanyia kazi 
Maafisa wa uhamiaji nchini UGANDA wamewakamata raia 28 wa CHINA kwa madai ya kuishi na kufanyakazi nchini humo kinyume cha sheria.

 
Raia hao wa CHINA wamekamatwa wakati maafisa wa uhamiaji walipovamia makao ya kampuni moja ya ujenzi ya CHINA ambapo baadhi yao walikutwa wamejifungia vyumbani kwa kuhofia kukamatwa.

 
Kampuni hiyo ya China Railway, ilikuwa imeshinda zabuni ya kujenga barabara ya karibu kilomita 100 eneo la KYEBANDO, mashariki mwa UGANDA.

Kampuni za kichina ni wawekezaji wakubwa barani AFRIKA, lakini zinalaumiwa kwa kushindwa kutoa ajira kwa wenyeji au kuwafanyia vitendo vya unyanyasaji.

No comments:

Post a Comment

Adbox