Wanaodaiwa kuhusika na utafunaji wa mabilioni hayo, walitumia mabadiliko mapya ya usajili wa vitambulisho, yaliyoigharimu serikali kupitia manunuzi yasiyo na tija huku wadanganyifu wakitumia mianya iliyopo kujinufaisha wenyewe kinyume na taratibu.
Kutokana na hali hiyo, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
(CAG) Profesa Mussa Assad, aliagiza wale vote waliohusika na ubadhirifu
na udanganyifu wa mabilioni ya fedha, wachukulie hatua kali.
“Ukaguzi umejiridhisha kwamba, uongozi, wafanyakazi, watoa huduma na wazabuni wameshiriki kwa namna moja au nyingine katika ubadhirifu na udanganyifu kwenye matumizi ya fedha katika mradi wa kuboresha vitambulisho vya taifa,” alisema.

Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)
imeonesha ubadhirifu katika eneo la usajili na utambuzi ambako Sh
bilioni 1.2 zililipwa kwa huduma za bima kupitia dalali wa Bima M/s Aste
Insurance Brokers Company Limited. Kiasi hicho kililipwa zaidi ya
gharama halisi isivyostahili.
Huduma hizi zilipaswa kugharimu Sh milioni 450.2, lakini mamlaka
ililipa Sh bilioni 1.7. CAG alibaini kuwa dalali huyo wa bima, alitumia
akaunti za biashara katika kupokelea fedha za malipo ya bima ya Sh
bilioni 1.7 badala ya akaunti ya amana isivyostahili.
Kwa hali hiyo, CAG amependekeza kampuni ya uwakala wa bima irejeshe
Sh bilioni 1.2 zilizolipwa zaidi isivyostahili; na hatua stahiki
zichukuliwe dhidi ya Astery Ndege na kampuni hii kwa kufanya udanganyifu
na kujipatia fedha kutoka mamlaka.
Ubadhirifu mwingine alioutaja ulikuwa ni manunuzi ya bima ya vifaa
vya usajili na magari yaliyotumika katika mradi wa vitambulisho vya
Taifa ya jumla ya Sh milioni 494, yaliyofanyika bila kukihusisha Kitengo
cha Manunuzi.
CAG pia ameshauri hatua stahiki zichukuliwe dhidi ya watumishi
waliohusika katika udanganyifu, uliobainishwa na kutozingatia sheria za
manunuzi ya umma na kuisababishia Mamlaka gharama zisizo na tija sanjari
na kuhakikisha kuwa wahusika wanafidia hasara iliyopatikana, kisha
kuhakikisha udhibiti wa vifaa.
Uhakiki wa leja za mafuta, pia ulibaini kuwa lita 1,110 za mafuta ya
dizeli yenye thamani Sh milioni 2.2 zilitumika kwa shughuli zisizo za
Mamlaka.
Pia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ilikopa Sh milioni 455.3
kutoka NIDA kwa ununuzi wa magari manne mwaka 2014, ambazo hadi ukaguzi
unafanyika Oktoba 2016 fedha hizo hazikuwa zimerejeshwa.
Uhakiki wa fomu zenye ‘Barcode’ zilizotengenezwa kupitia mpiga chapa
binafsi M/s MFI Solution, ulibaini kuwa fomu 7,762,907 zenye thamani ya
Sh bilioni 2.5 zilizopokelewa na mamlaka hazikutumika.
Kadhalika, ilibainika kuwa fomu 8,220,000 zenye thamani ya Sh
milioni 519.6 zilizochapishwa tangu mwaka 2011/2012 hadi 2013/2014
hazikutumika; hivyo kutelekezwa katika stoo za TANITA.
“Hali hii ilitokana na mamlaka kutokuwa na Mpangokazi, hivyo kuingia hasara ya Sh milioni 932.8,” ilisema ripoti hiyo.
Matengenezo ya magari
Aidha, kwa kipindi cha mwaka 2012/2013 mpaka 2015/2016, Mamlaka ilifanya matengenezo ya magari kupitia gereji binafsi yaliyogharimu Sh bilioni 1.3. Nida pia ilifanya matengenezo yaliyogharimu Sh bilioni 1.1 yaliyofanyika na kulipwa na Mamlaka bila kufanyika ukaguzi unaothibitisha kuwapo kwa ubovu wa gari na mahitaji ya matengenezo husika.

Pia kulikuwa na matengenezo yaliyogharimu Sh milioni 197.2,
yaliyofanyika na kulipiwa na Mamlaka bila kufanyika ukaguzi wa awali
wala ukaguzi baada ya matengenezo.
Ripoti imeeleza kuwa ukaguzi ulibaini malipo ya Sh milioni 42.7
yalifanyika zaidi ya madai stahili kutokana na udanganyifu wa kuongeza
tarakimu katika hati za madai na kutumiwa kwa hati moja ya madai zaidi
ya mara moja katika malipo ya kuanzia mwaka 2012/2013 hadi 2015/2016.
Ajira za muda na za kudumu
NIDA imegundulika kuwa ilikiuka sheria katika ajira za muda na za kudumu, zilizofanywa na mamlaka kuanzia mwaka 2012 hadi 2015, ambapo vibarua 1,071 walipatikana kwa kupigiwa simu bila kutangaza mahali popote kinyume na Sera ya mamlaka hiyo. Ukaguzi ulibaini kuwa NIDA iliomba kupatiwa vibarua kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu na Chuo cha Utumishi wa Umma wapatao 415.

Lakini baada ya kupatiwa vibarua hao, mamlaka haikuwatumia na
kubainisha kwamba wangetumiwa siku za baadaye. Ripoti ilifafanua kuwa
mamlaka iliamua kuajiri vibarua wengine wapatao 882 bila kutangaza
mahali popote, tofauti na watumishi 415 ambao walikwishapatiwa. Pia
Septemba 2015 Mamlaka iliajiri watumishi 213 licha ya kibali cha kuajiri
kutoka Utumishi kuisha tarehe Aprili 2015.
NIDA pia inatuhumiwa kufanya malipo Sh milioni 16.6 ya kiinua
mgongo kwa vibarua, kinyume na mkataba wa ajira ya muda na Sheria ya
Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka 2004.
Ubadhirifu mwingine uligundulika kwenye matumizi ya mafuta ya dizeli
na petroli, yaliyonunuliwa na mamlaka yenye thamani ya Sh bilioni 2.3,
yaliyotolewa kwenye magari na majenereta, ambapo hayakuthibitika
matumizi yake kutokana na sababu mbalimbali.
CAG pia amebaini upotevu wa vifaa vyenye Thamani ya Sh milioni 93.7
katika stoo ya mamlaka. Ukaguzi umebaini kuwa hakukuwa na taarifa rasmi
kutoka kwa mtunza stoo juu ya upotevu huo, licha ya kufahamu kuhusu
upotevu wa vifaa hivyo. Vifaa vyenye thamani ya Sh milioni 991.4
havikutumika tangu kununuliwa kwake katika vipindi tofauti kuanzia Machi
2013 hadi Oktoba 2016.
Udanganyifu mwingine ulifanyika katika ushindanishi wa wazabuni
katika ununuzi wa vifaa vya TEHAMA. Nida ilifanya manunuzi ya Ipad zenye
thamani Sh milioni 63.4 zilizonunuliwa kutoka kwa M/s Elite computers
baada ya kuonekana kukidhi vigezo vya ushindani na kupewa zabuni saba
(7) tofauti. Lakini taarifa za wazabuni ambao waliainishwa kuwa
washindani katika zabuni hii, M/s Prudent Enterprise na M/s Morex
General Enterprise zilighushiwa; na wazabuni hawa hawakuhusishwa wala
kutoa nukuu za bei.
Upangishaji nyumba Mamlaka ilitoa zabuni ya kuipangisha Ofisi ya
Mamlaka kwa Mary Mwema kupitia barua ya maombi ya tarehe 06.05.2012
ambapo tangazo la zabuni husika ni la tarehe 25.05.2012 baada ya tarehe
ya kuomba.
“Zabuni husika haikupitia Kitengo cha Manunuzi na haikuwa imeidhinishwa na Bodi ya Zabuni,” inasema ripoti hiyo.
Pia ripoti ilifafanua kuwa mzabuni wa upangishaji wa jengo la ofisi ya John Masenga haukujumuishwa kwenye mchakato wa tathmini ya kitaalamu licha ya kukidhi vigezo.
Pia ripoti ilifafanua kuwa mzabuni wa upangishaji wa jengo la ofisi ya John Masenga haukujumuishwa kwenye mchakato wa tathmini ya kitaalamu licha ya kukidhi vigezo.
No comments:
Post a Comment