NA JOHN WALTER MANYARA
Wakazi wa kijiji cha Matufa kata ya Magugu wilayani Babati mkoani Manyara wameliomba jeshi la polisi kuwashughulikia watuhumiwa waliokamatwa kwa kumbaka msichana mmoja mwenye miaka 23.
Msichana huyo alibakwa na kundi la wanaume tarehe 3/4/2017 wakati akitokea dukani majira ya saa 2:00 usiku na kusababishiwa maumivu makali katika sehemu zake za siri.
Akizungumza na Mwandishi wa habari hii biti huyo amesema ”alitokea kijana mmoja akanishika mkono huku akinivuta kwa nguvu na nikamuuliza kwanini unanishika kwa nguvu alinitukana na kuendelea kunivuta akinieleza kuwa nisibishane nae nitajua tu kinachofuata”.
Anasema alivutwa mpaka kwenye miti mingi ya mijohoro na kuanza kuvuliwa nguo kwa nguvu na watu waliokuwa zaidi ya sita na kuanza kumbaka huku akizibwa mdomo na kushikwa miguu.
Anaeleza kuwa alijaribu kupiga kelele ambapo msamaria mwema aliekuwa akipita alifika kumwokoa na kufanikiwa kukimbia hali ya kuwa tayari ameshabakwa na kupata maumivu makali sehemu zake za siri
Mwenyekiti wa kitongoji cha Kichangani Doglas Chasusa ni miongoni mwa watu waliofanya doria usiku kuwatafuta waliofanya uhuni huo anazungumzia tukio hilo
Kwa upande wa Baba wa msichana aliebakwa anasema binti yake alienda dukani ila cha kushangaza alichelewa kurudi nyumbani lakini hakupata wasi wasi kwa kuwa ni mkubwa na alishapazoea lakini alishangazwa kumkuta binti yake mlangoni akiwa amezimia hali iliyompa mshtuko ndipo waliponmpepea na baadae alipozinduka akaelezea kilimchompata huku akishindwa hata kukaa kwa maumovu makali aliyokuwa akihisi.
Akielezea namna alivyomwokoa binti huyo Shabani Bello anasema ilikuwa ni vigumu sana kwake kumwokoa lakini alitumia ujasiri wake kuwatisha lakini walimvamia na kujeruhi kichwani kwa rungu ndipo akapata nafasi ya kumbana mmoja na wengine wakakimbia.
Binti alipata majeraha mabaya sana na hata kutenguka mkono hali iliyomlazimu kwenda hospitali kufanyiwa vipimo.
Daktari aliekuwepo zamu usiku huo katika kituo cha afya Magugu Abbas Abdala , baada ya kumpima alithibitisha kwamba binti huyo kubakwa .
Hata hivyo Polisi waliwakamata watuhumiwa hao sita waliodaiwa kumbaka msichana huyo, na mpaka sasa wanashikiliwa kwenye kituo cha Polisi Magugu.
Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara Francis Jacob Masawe amethiubitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa watafikiswa mahakamani muda wowote.
Tukio kama hili liliwahi kutokea tena katika kijiji cha Matufa ambapo mama wa miaka 36 alibakwa na kundi la watu wasiofahamika hadi kufariki.
No comments:
Post a Comment