Hayo yameelezwa na tovuti ya habari ya Garowe na kuongeza kuwa, basi la abiria jana Jumapili lilikanyaga bomu hilo lililokuwa limetengwa barabarani katika eneo la Garasbaley, yapata kilomita 9 magharibi mwa Mogadishu na kusababisha maafa hayo.
Mashuhuda wa mripuko huo wamesema kwamba, hujuma hiyo ilikuwa imelenga msafara wa magari ya jeshi ambao ulikuwa unapita katika eneo hilo. Habari zaidi zinasema kuwa, waliojeruhiwa katika shambulizi hilo akiwemo mwanamke mmoja wanatibiwa katika hospitali moja mjini Mogadishu. Shambulio jingine la al-Shabaab mjini Mogadishu hivi karibuni
Magaidi wa al-Shabaab wamekuwa wakifanya mashambulizi dhidi ya misafara ya magari jeshi na Kikosi cha Kusimamia Amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM inayotumia barabara kuu ya Mogadishu kuelekea katika wilaya ya Afgoye na maeneo mengine ya nchi.

No comments:
Post a Comment