Jopo la madaktari bingwa wa Shirika la Stemm la Marekani kwa kushirikiana na Serikali,
limeamua kuwapeleka Marekani kwa matibabu majeruhi watatu wa ajali ya wanafunzi wa shule
ya Lucky Vicent iliyoua wanafunzi 32, walimu wawili na dereva.
Majeruhi hao ambao wamelazwa katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru ni Jofrey Tarimo,
Doreen Mshana na Sadia Awadh wanatarajiwa kusafirishwa kwenda Marekani wakiambatana na
wazazi wao, daktari na muuguzi wa hospitali ya mkoa wa Arusha.
Matibabu hayo yatatolewa kwa ufadhili wa madaktari hao kutoka Marekani ambao walikuwa
miongoni mwa watu wa kwanza kuwasidia wanafunzi hao kutoka kwenye gari lililo pata ajali,
wakiwa njiani kuelekea Ngorongoro na Serengeti kutalii.
Daktari mkuu wa hospitali Mount Meru, Wonanji Thimos amesema kuwa Serikali kwa
kushirikiana na madaktari hao imeshaanza taratibu za kuwasafirisha majeruhi hao kwa ajili ya
matibabu zaidi.
by Mussa Juma,Mwananchi
No comments:
Post a Comment