Rais wa Korea Kusini ahoji mfumo wa ulinzi wa Marekani

Amesema kuwa angependelea kutembelea Pyongyang katika hali nzuri.
Wakili huyo wa haki za kibinaadamu anayejulikana kwa maoni yake huria anataka kuimarisha uhusiano na Korea Kaskazini kinyume na sera iliopo kwa sasa.
Pia ameapa kuliunganisha taifa hilo linalokabiliwa na ufisadi ambao ulisababisha mtangulizi wake kushtakiwa mbali na kuimarisjha uchumi.
![]() |
Rais mpya wa Korea Kaskazini Moon Jae-in ameapishwa rasmi |
Mwanachama huyo wa chgama cha Democrat amejionyesha kuwa mtu ambaye anaweza kuliendesha mbele taifa hilo kutoka kwa ufisadi mbali na kuliunganisha.
Uongozi wa bwana Moon utaangaliwa huku kukiwa na wasiwasi mwingi katika eneo hilo.
Marekani na Korea Ksakazini zimekabiliana kimaneno katika majuma ya hivi karibuni baada ya Pyongyang kufanya majaribio ya makombora
BBC Swahili
No comments:
Post a Comment