LATEST NEWS

Wednesday, August 9, 2017

Ezekiel Kemboi hatimaye amestaafu mbio za kuruka maji na viunzi

Baada ya umaarufu katika ulingo wa riadha duniani kwa miaka 16 yaliyopita, mwanariadha Ezekiel Kemboi, anayefahamika sana kwa ubabe wake katika mbio za mita 3000 kuruka maji na viunzi hatimaye amestaafu mbio hizo.

Kemboi aliyeshinda medali nyingi katika mbio hizo, badala yake ametangaza kuwa ataanza kushiriki mbio za marathon kuanzia sasa kusonga mbele

Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 35 na ambaye anahudumu kama afisa wa polisi katika kitengo cha kusindikiza rais, alimaliza wa 11 kwa fainali za mwaka huu katika mashindano ya dunia yanayoendelea jijini London Jumanne usiku katika mbio zilizoshindwa na Mkenya mwenzake Conseslus Kipruto.

Kemboi anajivunia kuwa mwanariadha wa pekee kushinda mataji ya dunia nne mtawalia katika mbio hizo pamoja na kutwaa medali mbili za dhahabu za Olimpiki.

Akizungumza na wanahabari jijini London, Kemboi alisema mbio za jana zilikuwa za mwisho kwake na akadhibitisha kuwa kuanzia mwezi Aprili mwakani, atajitosa katika mbio za masafa marefu au marathon.

No comments:

Post a Comment

Adbox