LATEST NEWS

Wednesday, August 9, 2017

Kocha wa Rwanda atarajia ushindi dhidi ya Uganda




Baada ya kushuhudia ushindi wa timu yake dhidi ya timu ya taifa ta soka ya Sudan 2-1 katika mechi ya kirafiki uwanjani Kigali, kocha mkuu wa Amavubi Antoine Hey ameelezea imani kuwa kikosi chake kitaweka tabasamu katika nyuso za Warwanda timu hiyo itakapochuana na Uganda katika mashindano ya kufuzu Kombe la Afrika CHAN jumamosi.

Hey amesema mchuano huo wa kirafiki uliwapa taswira kamili kuhusu wachezaji gani watacheza dhidi ya Uganda na kusema kuwa anataraji uzoefu uliopatikana utasaidia timu hiyo itakapopambana na Uganda katika uwanja wa St. Mary's College Kitende jijini Kampala.

Timu hiyo ya taifa itaelekea Uganda hapo kesho tayari kwa mchuano wa jumamosi ambao utaamua ni nani ataingia fainali za kombe la Afrika CHAN itakayoandaliwa Kenya mwakani. Hey hata hivyo anasema timu yake iko katika hali nzuri kufuzu mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment

Adbox