Baada ya ngoja ngoja, hatimaye msimu wa 2017-18 ya primea ya Uingereza utarejea leo usiku wakati Arsenal inajiandaa kuwa mwenyeji wa Leicester City katika uwanja wa Emirates. Hii itakuwa mara ya kwanza kwa ligi hiyo kuanza siku ya Ijumaa.
Arsene Wenger atakuwa meneja wa kwanza kuifunza timu inayoshiriki ligi ya primea kwa misimu 22 tofauti.
Vilabu vya Uingereza vinaanza msimu huu baada ya kufanya ununuzi wa wachezaji kwa njia isiyo ya kawaida kwani vimetumia ada nyingi mno kupata wachezaji waliowamezea mate.
Kufikia tarehe 10 Agosti, siku moja kabla ya kuanza kwa ligi hiyo, timu hizo zilikuwa zimewekeza jumla ya pauni bilioni 1.034 kwa wachezaji wapya ambayo inamaanisha ligi hiyo itapitisha kiwango cha pesa kilichotumiwa msimu wa uamisho wa mwaka jana wa pauni bilioni 1.165, wiki tatu zikiwa zimesalia kufunga dirisha la uamisho.
No comments:
Post a Comment