LATEST NEWS

Friday, August 11, 2017

Mashindano ya magari ya Mt. Gorilla kuanza mwezi ujao

Mashindano ya magari ya mwaka 2017, Africa Rally Championship (ARC) itaelekea Rwanda mwezi ujao wakati Mountain Gorilla Rally itakapoanza Septemba 8-10. Mkondo wa Rwanda ni katika raundi ya sita katika kalenda ya mashindano ya magari inayojumulisha raundi saba.

Madereva wa nyumbani, eneo na barani kwa ujumla wanatarajiwa kushiriki mashindano hayo ya Rwanda ambayo imekuwa vigumu kutabiri itakavyokuwa.

Kwa madereva wa nyumbani, itakuwa nafasi ya kutafuta kujizolea pointi kabla ya kuanza kwa mashindano ya magari ya kitaifa.

Lakini kwa mashabiki wa nyumbani wa mashindano hayo, hii itakuwa wakati wa kusisimua kuwaona madereva kama vile Giancarlo Davite wakiendesha Rwanda baada ya kupigwa marufuku kushiriki mashindano hayo kwa mwaka mmoja.

No comments:

Post a Comment

Adbox