LATEST NEWS

Wednesday, August 9, 2017

TEF WAONDOA ZUIO LA KUTOKUTOA HABARI ZA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM, MAKONDA.

JUKWAA
la wahariri Tanzania (TEF) laondoa zuio la kutokutoa habari za Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Mkonda jijini Dar es Salaam leo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,
Mwenyekiti
wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Theophil Makunga amesema kuwa "
Mgogoro huu kati ya Jukwaa la wahariri wa habari na tasnia ya habari na
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Mkonda umefika mwisho tunarusu sasa
habari zake ziandikwa mgogoro ule uliokuwepo yaliyopita si ndwele tugange yajayo"
 
Tamko hilo la TEF
limekuja mara baada ya Machi 22 mwaka huu kutoa tamko lao kwa vyombo
vya habari lililokuwa likisema "Zinalaani vikali vitendo vya Mkuu wa
Mkoa katika kuvamia chombo cha habari cha Clouds Media akiwa ameambatana
na Askari wenye silaha.



Mwenyekiti
wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Theophil Makunga akizungumza na
waandishi wa habari pamoja na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari
jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuondoa adhabu aliyopewa Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambayo alikua nayo ikiwa Jukwaa hilo la
wahariri lilimfungia kwa kutokutoa habari yoyote kutoka kwa Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Vipindi na uzalishaji wa
Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.



Kulia
ni Mkurugenzi wa Vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge
Mutahaba akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo
wakati wa Jukwaa la wahariri kuondoa zuio kutotoa habari zamkuu wa ,Mkoa
wa Dar Es Salaam leo.




Kulia
ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na waandishi
wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati Jukwaa la wahariri Tanzania
(TEF) wakiondoa zuio la kutokutoa habari yoyote kwenye chanzo cha Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam kwenye vyombo vya habari sasa kuanzia leo
habari za mkuu wa Mkoa wa Mkoa zitakuwa zikitoka kwenye vyombo vya
habari. katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri
Tanzania(TEF), Deodatus Balile na kushoto ni Mkurugenzi wa Vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.



Katikati ni Makamu
Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Tanzania(TEF), Deodatus Balile
akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
leo. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kushoto ni Mkurugenzi wa Vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.

No comments:

Post a Comment

Adbox