LATEST NEWS

Thursday, August 10, 2017

WAHALIFU 13 WAUAWA NA POLISI KIBITI



Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akipata maelezo kutoka kwa
Mkuu wa Operesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi
(DCP) Liberatus Sabas kuhusiana na tukio la kuuawa wahalifu 13 katika
majibizano ya risasi baina ya Polisi na wahalifu hao katika eneo la
Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti. Chini
ni silaha 8 aina ya SMG pamoja na vifaa vingine zilizopatikana katika
majibizano hayo. – Picha na Jeshi La Polisi.



Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akionesha makasha ya
risasi (magazine) ambazo ni miongoni mwa makasha 8 yaliyokuwa
yakitumiwa na wahalifu katika eneo la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni
Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti. Wa kwanza kushoto ni Kamishina wa
Polisi Jamii (CP) Mussa Alli Musa akifuatiwa na Mkuu wa Operesheni
Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus
Sabas. Katika tukio hilo Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwaua wahalifu 13
ambao walikuwa wakifanya mauaji Kibiti. – Picha na Jeshi La Polisi.


Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akielezea baadhi ya vitu
mbalimbali vilivyokuwa vikitumiwa na wahalifu 13 waliouawa katika eneo
la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti
ambapo jumla ya silaha 8 aina ya SMG, risasi 158, pikipiki 2, pamoja
na begi la nguo vilivyokuwa vikitumiwa na wahalifu hao. Kushoto ni
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya jinai (CP) Robert Boaz.


Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akionesha silaha aina ya
SMG ambayo ni miongoni mwa silaha 8 zilizokuwa zikitumiwa na wahalifu
13 waliouawa katika majibizano ya risasi baina yao na Jeshi la Polisi
katika eneo la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa
ya Kibiti. Wa kwanza kulia ni Kamishina wa Polisi Jamii (CP) Mussa Alli
Musa akifuatiwa na Mkuu wa Operesheni Maalumu za Jeshi la Polisi,
Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas. – Picha na Jeshi La
Polisi.


Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akiongea na wananchi wa
Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti alipokuwa akitoka
kukagua eneo la tukio walipouawa wahalifu 13 katika majibizano ya
risasi baina yao na Jeshi la Polisi katika eneo la Tangibovu.

(Picha na Jeshi La Polisi.)

Tarehe 04.08.2017 huko eneo la Gari Bovu,
kijiji cha Chamiwaleni, Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti, Wilaya ya Kibiti, Mkoa
wa Kipolisi Rufiji, Jeshi la Polisi lilimkamata Abdallah Abdallah Mbindimbi @Abajani akiwa ana majeraha maeneo
mbalimbali ya mwili wake akionekana kuwa alikuwa anaendelea kujitibia mwenyewe
kwa njia za kificho. Mtuhumiwa huyu, alikamatwa kutokana na kuwepo kwa taarifa
za kiintelijensia kuhusu yeye kuhusika na vitendo vya kufadhili, kusaidia,
kuhifadhi na kushiriki uhalifu wa ujambazi maeneo mbalimbali. Mtuhumiwa alipohojiwa
kuhusiana na tuhuma zinazomkabili alikubali na alionyesha dhamira ya kwenda
kuonyesha Ngome yao.











Tarehe 09.08.2017 majira ya saa 21:00 Hrs (saa tatu usiku) katika mapori ya kijiji cha Rungungu mtuhumiwa
akiambatana na Askari Polisi alikwenda kuonyesha Ngome ya watuhumiwa wenzake aliokuwa
anashirikiana nao kufanya uhalifu. Baada
ya kukaribia eneo la tukio ulitokea upinzani mkali wa majibizano ya risasi
jambo lililopelekea hata Abdallah
Abdallah Mbindimbi @Abajani kujeruhiwa na risasi sehemu mbalimbali za mwili
wake. Kufuatia majibizano hayo, Askari Polisi walifanikiwa kuwajeruhi wahalifu 12
(kumi na mbili. Jitihada zilifanyika kuwapeleka Hospitali majeruhi wote 13
(kumi na tatu) ingawa baadae walifariki dunia kwa nyakati tofauti wakipelekwa
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutokana na kuvuja damu nyingi zilizosababishwa
na majereha ya risasi sehemu mbalimbali za miili yao. Miili ya marehemu
imehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
Jijini Dar es salaam.

Ndugu Wanahabari

Watuhumiwa
7 (Saba) kati ya 13 (kumi na tatu) waliopoteza
maisha kutokana na majibizano ya risasi
wametambuliwa kuwa ni:

1. Hassani Ali Njame

2. Abdallah Abdallah Mbindimbi @
Abajani

3. Saidi Abdallah Kilindo

4. Abdulshakuru Mohamed Ubuguyu

5. Issa Mohamed Mseketu @Mtawa

6. Rajabu Thomas @Roja

7. Mohamed Ally Kadude @Upolo

Miili
6 (sita) iliyobaki haikuweza
kutambulika mara moja hivyo utambuzi utaendelea huko ilikohifadhiwa Hospitalini
DSM.

Ndugu
Wanahabari

Vielelezo mbalimbali
vilipatikana katika eneo la tukio, kama ifuatavyo:





S/N



KIELELEZO



UTAMBUZI





SILAHA, RISASI NA MABOMU





1.



SMG = 5



Mali ya Jeshi la
Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani





2.



Anti Riot Gun 38mm
= 2



Mali ya Jeshi la
Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani





3.



SAR = 1



Mali ya Jeshi la
Polisi tukio la kupora Silaha Askari Polisi huko Stakishari Jijini Dar es
Salaam





4.



MAGAZINI = 2



Mali ya Jeshi la
Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani





5.



Risasi za SMG 158



Mali ya Jeshi la
Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani





6.



Bomu la kurusha kwa
mkono = 1



Uchunguzi dhidi ya
Bomu hilo unaendelea





7.



Mabomu ya kutuliza
ghasia = 4



Mali ya Jeshi la
Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani





VIELELEZO VINGINE





8.



Pikipiki = 2



Pikipiki hizi
zilitumika kuwasafirisha wahalifu hawa kwenye utekelezaji wa matukio ya
uhalifu maeneo mbalimbali





9.



Vitenge na Nguo
mbalimbali



Vitenge na nguo
mbalimbali viliporwa baada ya kufanya tukio la kumuua Diwani wa Zamani wa Kibwiwi


10.




Begi = 1



Liliporwa baada ya
kumuua Mtendaji wa Kijiji cha Mangwe


Ndugu Wanahabari

Kwa
mujibu wa taarifa za utambuzi wa vielelezo vilivyopatikana eneo la tukio na
utambuzi wa baadhi ya miili ya watuhumiwa waliofariki inaonyesha kuwa walishiriki matukio ya uhalifu
maeneo mbalimbali kama ifuatavyo:

1.
Kuua
OC CID na Watumishi 2 (Wawili) wa Idara ya Maliasili katika tukio la Jaribu
Mpakani – Wilaya Kibiti

2.
Kuua
Askari Polisi 8 (Nane) katika tukio la Mkengeni – Wilayani Kibiti

3.
Kuua
Trafiki 2 (Wawili) katika tukio la Bungu “B” – Wilaya ya Kibiti

4.
Kumuua
Diwani wa Zamani CCM katika tukio la Kibwibwi – Wilaya ya Kibiti

5.
Kuua
Afisa Mtendaji, Mwenyekiti wa Mtaa na
Mkulima katika tukio la Kijiji cha Mangwi – Wilaya ya Kibiti

Ndugu
Wanahabari

Wito wangu kwa Wananchi
ni kuhusu mambo muhimu yafuatayo:

a.
Wananchi wote nchini kuondoa hofu ya
kwamba eneo hili si salama. Nawaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa
Jeshi la Polisi na kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha nawaomba
wananchi kutoa taarifa mara moja kwa Jeshi la Polisi wanapohisi kuna jambo lolote wanalolitilia
mashaka.

b.
Natoa wito kwa wananchi wa mkoa wa
Pwani, hususani maeneo ya Mkuranga, Kibiti na Ikwiriri, kuendelea na shughuli zao
mbalimbali za kujiletea maendeleo. Nawasihi kwa dhati kabisa waendelee
kutupatia taarifa zitakazosaidia kumaliza kabisa uhalifu kwenye eneo hili. Nitumie
fursa hii kuwashukuru sana wananchi wa maeneo ya Mkuranga, Kibiti na Ikwiriri
kwa ushirikiano mnaotupatia ambao umesaidia sana kuwadhibiti wahalifu.

c.
Mamlaka za Hospitali, Zahanati, Vituo
vya Afya, Maabara za Afya ya Binadamu na Maduka ya Kuuza Dawa za kutibu Binadamu
zijiepushe na utaratibu wa kutoa matibabu kienyeji au kificho kwa watu
waliojeruhiwa bila kufuata taratibu za kisheria ikiwemo kupata taarifa ya
Polisi “kupitia Fomu maalum ya kuruhusu
matibabu (maarufu kama PF. 3)”. Wahalifu wakijeruhiwa ni lazima watafute
matibabu.

Kwa
hiyo idara hizi ni muhimu sana kutoa ushirikiano ili kutuwezesha kuwakamata watuhumiwa
maana baadhi yao wamekutwa na majeraha sehemu mbalimbali za miili yao na
walikuwa wanaendelea kujitibia kwa kificho kwa kutumia dawa za hospitali. Natoa
wito kwa Mamlaka hizo kutoa taarifa mara moja kwa Jeshi la Polisi wanapoona ama
kumbaini mtu ambaye ataonekana kuwa na majeraha na anatafuta tiba bila ya
kufuata taratibu.

Ndugu
Wanahabari

Napenda kuujulisha Umma
kwamba wapo baadhi ya Watuhumiwa,
Wafadhili na Washirika wa Uhalifu na Wahalifu wa ujambazi maeneo haya ambao
bado hawajakamatwa. Jambo la kufurahisha ni kwamba taarifa zao zipo kwa Jeshi
la Polisi nchini na zinaendelea kufanyiwa kazi ili waweze kukamatwa na kufikishwa kwenye mkono wa
Sheria mara moja.

Natoa wito kwa
wananchi ambao wanawafahamu watuhumiwa wafuatao kutoa taarifa katika kituo
chochote cha Polisi ili waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria. Picha
za watuhumiwa hao zitasambazwa kote nchini ili iwe rahisi kuwabaini. Majina ya watuhumiwa
hao ni:

i.
Anafi
Rashid Kapelo @ Abuu Mariam

ii.
Hassan
Haruna Kyakalewa @ Abuu Salma @ Shujaa @ Dokta

iii.
Haji
Ulatule

iv.
Shekhe
Hassan Nasri Mzuzuri

v.
Rashid
Mtutula


Ndugu
Wanahabari

Nimalizie kwa kusema
kwamba uhalifu kwenye eneo hili ni suala la muda mfupi. Na tunaendelea vizuri
sana. Hali ya usalama imeimarika sana eneo hili. Nazidi kutoa wito kwa wananchi
kuendelea kuliunga mkono Jeshi la Polisi ili kufikia malengo yake ya kuzuia, kubambana na kutanzua uhalifu
nchini.


Imetolewa
na;


Simon Nyakoro Sirro

Inspekta Jenerali wa Polisi

IKWIRIRI

10.08.2017

No comments:

Post a Comment

Adbox