MKUU wa Wilaya ya Singida amepiga marufuku wafanyabiashara wa vitunguu kutoka nchi jirani za Kenya,Uganda,Ruanda,Burundi,Zambia, Kongo na Malawi kwenda kununu vitunguu kweneye mashamba ya wakulima vijijini na badala yake amewataka kwenda kununua kwenye soko la kimataifa la vitunguu,lililopo Manispaa ya Singida.
Zuio lilitolewa na Mkuu wa wilaya ya Singida,Bwana Eliasi Tarimo baada ya kupokea malalamiko ya wafanyabiashara kutoka soko la kimataifa la vitunguu, kulalamikia kuwa wafanyabiashara wanaotoka nchi hizo kuwa wanakwenda kununua vitunguu kwenye mashamba ya vijijini na hivyo kusababisha biashara katika soko hilo kudorora huku serikali ikikosa mapato yake.
Nao baadhi ya wafanyabiashara wa vitunguu katika soko hilo la kimataifa,Bwana Jonathani Mpinga amesema kuwa serikali haina budi kuweka usawa wa sheria ya kuzuia ujazaji kwa njia ya lumbesa kwa mikoa yote badala ya sheria hiyo kutumika katika Mkoa wa Singida peke
No comments:
Post a Comment