Thursday, March 30, 2017

RC PWANI APIGA MARUFUKU BODA BODA KUFANYA KAZI USIKU

 
Na, Onesmo Loi

Kutokana na kukithiri kwa matukio ya uhalifu na mauaji, Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Pwani imesitisha usafiri wa bodaboda muda wa jioni wilayani Rufiji kuanzia saa 12:00 jioni hadi saa 12:00 asubuhi.

Akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Pwani  Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo amesema hatua hiyo inatokana na watuhumiwa wa uhalifu kutumia usafiri huo na matukio hayo kufanyika kati ya muda huo hadi saa mbili usiku.

Uamuzi huo umekuja siku mbili baada ya kuuawa kwa mjumbe wa Serikali ya Kijiji cha Ikwiriri Kaskazini, Emmanuel Alberto kwa kupigwa risasi akiwa nyumbani kwake, tukio hilo likifanya idadi ya viongozi wa Serikali za Mitaa na polisi waliouawa kufikia takriban 11 katika wilaya za Rufiji na Kibiti.

No comments:

Post a Comment

Adbox