Friday, March 31, 2017

Nchi za Pembe ya Afrika zaahidi uwekezaji zaidi kwenye miradi ya kukabiliana na ukame

Nchi za Pembe ya Afrika zimerejea tena ahadi yao ya kuongeza uwekezaji kwenye miradi ya kukabiliana na ukame ili kuwasaidia wanyoge kuepukana na uhaba wa chakula na maji.
 

Wabunge na wataalam kutoka Shirika la Kiserikali la Maendeleo la nchi za Afrika Mashariki (IGAD) wanaokutana mjini Nairobi, Kenya, wamesema uwekezaji wa kimkakati wa mapema, uelewa wa jamii, na mfumo wa kilimo unaozingatia mabadiliko ya hali ya hewa ni muhimu katika kudhibiti balaa la njaa, utapiamlo, na uhaba wa maji katika kanda hiyo.
 

Waziri wa Mipango na Ugatuzi wa Kenya Mwangi Kiunjuri amesema, maboresho ya teknolojia ya utabiri wa hali ya hewa, kufufua mfumo wa ikolojia na kuongeza uelewa wa umma ni muhimu katika kupunguza athari ya kujirudia kwa ukame katika kanda ya Pembe ya Afrika.

No comments:

Post a Comment

Adbox