
UZALISHAI wa mbegu bora za mazao mbalimbali ya kilimo nchini bado
ni changamoto kubwa kutokana na mbegu bora zinazozalishwa kutokukidhi mahitaji
ya soko linalotokana na ongezeko la wakulima wanaotumia mbegu hizo kwenye
kilimo. .
Hayo yameelezwa leo na Meneja wa Shamba la mbegu la serikali,
ASA,la mkoa wa Arusha, Zadiel Mrinji, alipokuwa akizungumza na wajumbe wa
baraza la wafanyakazi ambao ni wataalamu wa uzalishaji wa mbegu bora kutoka
mashamba yote tisa ya serikali yaliyopo kwenye kanda saba nchini,
Akifungua kikao cha baraza hilo, kilichofanyika ukumbi wa kituo
cha kulelea Yatima cha SOS,kilichopo Ngaramtoni , mkurugenzi wa masoko na
mashamba ya mbegu bora nchini, ASA, Philemon Kawamala, amesema ASA ina
majukumu manne ambayo ni pamoja na kuongeza uzalishaji wa mbegu bora
,kuhamasisha sekta binafsi kushiriki kwenye uzalishaji wa mbegu bora .
Kwa upende wake msaidi wa shamba la Arusha, ambaye pia afisa
killimo Marko Mwendo, amewashauri wakulima kuwa kutunza risti pindi wanunuapo
mbegu kutokakwa mawakala lengo ni kuwezesha kufuatilia iwapo kutakuwepo na
dosari kwenye mbegu hizo.
No comments:
Post a Comment