
Rais wa Marekani Donald Trump
ameliruhusu jeshi la nchi hiyo kuongeza mashambulizi zaidi nchini
Somalia kwa ajili ya kupambana na wanamgambo wa Al Shabab.
Hii
italifanya jeshi la Marekani kutumia nguvu zaidi sambamba na vifaa vya
kisasa kupambana na wana mgambo hao, huku pia wakitoa usaidizi wa karibu
kwa jeshi la Somalia.Inatarajiwa idadi kubwa ya wanajeshi wa Marekani wataelekea nchini Somalia kwa ajili ya operesheni hii.
Al Shabab wameendelea kufanya mashambulizi yanayosababisha vifo kila kukicha nchini Somalia na hata katika nchi jirani ya Kenya.
Source:BBC Swahili
No comments:
Post a Comment