Friday, March 31, 2017

Zuma amfukuza kazi waziri wa fedha Pravin Gordhan

Kwa siku za hivi karibuni Zuma amekuwa na ushawishi mdogo ndani na nje ya chama cha ANC Kwa siku za hivi karibuni Zuma amekuwa na ushawishi mdogo ndani na nje ya chama cha ANC


Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amewafukuza kazi mawaziri wake kadhaa akiwemo Waziri wa fedha Pravin Gordhan pamoja na naibu wake Jonas Mkabisi ambao ndio waliokua sababu kuu ya kuwepo mabadiliko haya.
Taarifa kutoka ikulu ya Afrika Kusini zinasema Malusi Gigaba ameteuliwa kuwa waziri mpya wa fedha.
Takriban mawaziri 15 wametimuliwa katika kile kinachotajwa kama mshangao kwa serikali ya Zuma.
 Aliyekuwa waziri wa fedha Pravin Gordhan Aliyekuwa waziri wa fedha Pravin Gordhan

Mapema wiki hii Gordhan aliamriwa kurudi nyumbani kutoka London alipokwenda kwa ziara ya kikazi, baada ya kutuhumiwa kuwa alikua akipanga njama za kuipindua serikali iliyopo madarakani.
Maafisa kadhaa kutoka chama tawala cha ANC wanapinga kuondolewa kwa Gordhan.
Source:BBC Swahili

No comments:

Post a Comment

Adbox