Naibu
Waziri Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni, akimuuliza maswali Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim
Mgandilwa, wakati alipotembelea Ujenzi wa Kituo cha Polisi Mjimwema,
Wilayani Kigamboni kukagua maendeleo ya ujenzi huo. Kulia ni Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke, Gilles Muroto na anayefuatia ni Mkuu wa
Utawala Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Benadict Kitalika
Mkuu
wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa, akimuonyesha eneo
linapotakiwa kujengwa kituo cha Polisi Kibada, Naibu Waziri Wizara ya
Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, wakati wa ziara
ya naibu waziri,wilayani Kigamboni, Dar es Salaam.
Naibu
Waziri Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni (kulia), akikagua moja ya chumba cha mahabusu ndani ya kituo cha
Polisi Mwasonga, wakati wa ziara ya ukaguzi wa vituo vya polisi
wilayani Kigamboni, jijini Dar es Salaam.Katikati ni Mkuu wa Wilaya
hiyo, Hashim Mgandilwa.
Muonekano
wa nje wa Kituo cha Polisi cha Mwasonga kilichopo wilayani Kisarawe,
kikiwa katika hatua za mwisho kabla ya ujenzi wake kukamilika.
Naibu
Waziri Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni, akizungumza na madereva bodaboda wakati wa ziara ya kikazi
wilayani Kigamboni ambapo aliwaasa madereva hao kufuata sheria za
usalama barabarani pindi wafanyapo shughuli zao ili kuepuka ajali.
Muendesha
Bodaboda wa Wilaya ya Kigamboni, Said Athumani, akimuuliza maswali
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni (hayupo pichani), wakati wa Mkutano ulioitishwa na naibu waziri
huyo wakati wa ziara ya kikazi wilayani humo.
Muendesha
Bodaboda wa Wilaya ya Kigamboni, Fredrick Swai, akimuuliza swali Naibu
Waziri Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
(hayupo pichani), wakati wa Mkutano ulioitishwa na naibu waziri huyo
wakati wa ziara ya kikazi wilayani humo. Picha na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment